Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na Balozi wa Marekani nchini, Michael Battle katika Ofisi Ndogo za Wizara, Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu maandalizi ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani nchini, Kamala Harris, masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Michael Battle katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Tax ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kushirikiano na Serikali ya Tanzania wakati wote tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo na umekuwa na maslahi mapana kwa wananchi wa pande zote mbili huku Balozi wa Marekani Nchini, Battle ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha uhusiano wake na Serikali ya Marekani.

Katika tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini, Andrey Avetisyan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam na kuipongeza kwa fursa za masomo inazozitoa kwa watanzania na kuomba ushirikiano katika sekta za kilimo, madini, afya na uhandisi.

Balozi wa Urusi nchini, Andrey Avetisyan akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Naye Balozi wa Urusi, Andrey Avetisyan amesema Serikali ya Urusi inategemea kuongeza idadi ya ufadhili wa nafasi za masomo kutoka idadi ya nafasi 90 hadi 120 ili kutoa nafadi zaidi kwa watanzania kunufaika na fursa za elimu zinazopatikana nchini Urusi.

Urusi imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali hususan sekta za elimu, afya, utalii na utamaduni, mafuta na gesi, ulinzi na usalama, madini, kilimo na uhandisi.

Kamati yaridhia mpango, Bajeti ofisi ya Waziri Mkuu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 23, 2023