Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema Tanzania na Marekani zitashirikiana kuhamasisha utoaji wa  Elimu ya afya kwa umma juu ya kujenga tabia ya kufanya mazoezi na lishe bora ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanakuwa kwa kasi sana nchini.

Ameyasema hayo leo Juni 16,2021 Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright kuhusu kukabiliana na tatizo hilo pamoja na mambo mengine yanayoigusa Wizara hiyo.

“Nimemwambia Balozi Donald kuwa  tayari Wizara yangu  inajadiliana na Wizara ya Afya kushirikiana kufanya kampeni endelevu nchi zima, Bara na Visiwani kuhusu ufanyaji mazoezi kwa wananchi,” amesema Bashungwa.

Bashungwa amesema kuwa nchi hizo zitaendelea ushirikiana kuendesha tasnia ya Sanaa na Michezo, ambapo Balozi wa Marekani Nchini amekubali ujumbe wa NBA kutoka Marekani kutembelea Tanzania mwaka huu kujadili maendeleo ya mchezo wa kikapu.

Biden, Putin wakutana uso kwa macho
Miaka 20 jela kwa kukutwa na meno ya Temba