Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Nchi ya Burundi hasa katika kuimarisha ulinzi katika mipaka ya nchi hizi mbili.

Amesema hayo wakati akizungumza na Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu.

“ Ujenzi wa reli ya kisasa, tumeendeleza mazungumzo ya mtandao wa kujenga reli kutoka Uvinza hadi Msongati Utega, kilomita 160 zipo Tanzania na kilomita 80 zipo Burundi, Congo nayo imeongeza kipande kutoka Uvira Burundi hadi Kindu DRC”.

Itakumbukwa Januari mwaka huu, nchi hizi tatu zilisaini makubaliano kupitisha mizigo bandari ya Dar es Salaam, Shehena za madini ya nickel kutoka Burundi hadi bandari ya Dar es salaam ili yaweze kusafirishwa kwenda masoko ya kimataifa Inakadiriwa tani 150 wastani wa tani milioni tatu hadi tano zitasafirishwa kupitia reli hiyo na Bandari ya Dar es Salaam.

Aidha, Tanzania inaungana na Jamhuri ya Burundi kulaani matukio ya kigaidi yaliyotokea tarehe 18 na 20 Septemba mwaka huu, yaliyosababisha vifo vya watu sita na wengine karibu 50 kujeruhiwa pamoja na uharibifu wa mali.

Ziara ya Rais Ndayishimiye ni mwendelezo wa hatua zinazochukuliwa na serikali zetu mbili kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika sekta mbalimbali kwa masilahi ya pande zote mbili za nchi zetu.

”Tulizungumza na Burundi pia na kuwajuza tuna huduma za Kibingwa katika maradhi ya kansa na maradhi ya moyo hivyo watumie nchi yetu kupata huduma hizo. Kwenye suala la Corona wenzetu wa Burundi wamejitahidi sana, wamekua na utaratibu wa kupima kila wiki, na kwenye hili pia tumepanga kushirikiana nao”.

“Tanzania tumeshatoa Leseni kwa Kampuni ya Kabanga Nickel ambapo hilo hilo litakuwa ni soko la Burundi kwa ajili ya madini yao pia.” amesema Rais Samia.

Muigizaji amuua mwenzie kwa risasi wakiwa Location
Twiga Stars yakamilisha maandalizi