Timu ya Tanzania Prisons ya Jijini Mbeya imeendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Jkt Tanzania, unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi (Machi 31, 2018) katika viwanja vya kumbukumbu Sokoine.

Hayo yamesemwa na kocha wa timu wa Tanzania Prisons, Mohammed Abdalla ambapo amesema kuwa kikosi chake kipo imara kutokana na kufanya mazoezi ya kutosha ambayo yamedumu kwa muda wa wiki mbili sasa.

Kwa upande wake nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile, amesema kuwa Timu ya JKT. Tanzania sio ya kubeza  kutokana na ushindani pamoja na ufundi wao uwanjani hivyo wamejipanga kuikabili.

Hata hivyo, Timu ya Tanzania Prison inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 36 nyuma ya Timu ya Azam Sport Club.

Ajali ya Basi yatokea Jijini Mbeya
Uganda yavifungia vituo vya redio 23.