Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametembelea Uwanja wa Nelson Mandela kujionea maandalizi yanayoendelea kufanywa uwanjani hapo, kwa ajili ya mchezo wa mzunguuko wa 18 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Young Africans utakaochezwa siku ya Alhamisi (Desemba 31).

Mh.wangabo amerishishwa na maandalizi ya Uwanja huo, na pia ametoa tahadhari kwa timu za Young Africans na Tanzania Prison kutoingia uwanjani na matokeo.

Amesema timu hizo mbili zilipokutana katika mzunguuko wa kwanza jijini Dar es salaam zilitoka sare ya 1-1 hali ambayo inawafanya vinara wa Ligi hiyo Young Africans kukamia kupata alama tatu ugenini huku wenyeji Tanzania Prison wataweka dhamira ya kutokua wanyonge katika uwanja wa nyumbani kwa kutokubali kufungwa.

Pia amewakumbusha wachezaji, viongozi na mashabiki wa timu hizo kuwa mchezo una matokeo matatu kufungwa, kushinda na kutoka sare, hivyo kila timu iwe tayari kupokea moja kati ya matokeo hayo.

 “Wapenzi wa mpira wa miguu wafike kwa wingi waweze kujione mshindi atakuwa ni nani, kwasababu mpira una matokeo matatu, kuna kushinda, kufungwa lakini pia kuna sare, timu zote mbili zijiandae kwa matokeo hayo matatu, isije mtu anakuja na matokeo yake hapa kwamba mimi nitashinda halafu akashindwa halafu akafanya fujo, sasa sisi vyombo vya ulinzi na usalama tumeshajiweka vizuri kwa fujo zozote ambazo mtu amejiandaa nazo aziache huko huko.” Amesisitiza.

Aidha ameongeza kuwa mpira ni furaha na pia ni urafiki ingawa kuna kushinda na kushindwa, hivyo amewataka mashabki kufika uwanjani hapo kutoka meneo tofauti ya ndani na n je ya mkoa Rukwa.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 30, 2020
Simba SC kuikaribisha Ihefu FC