Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe amedai kuwa Tanzania ya zamani ilikuwa ikiishi kama nchi yenye laana kutokana na baadhi ya rasilimali zake kutumika zaidi na wageni na kushindwa kuwafaidisha watanzania wenyewe.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini walipokuwa wakizungumza na Rais Dkt, John Pombe Magufuli ili kuhakikisha sekta hiyo inainua uchumi wa Tanzania.

Kakobe amesema kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu kwasababu amemuinua shujaa Rais John Pombe Magufuli ambaye amekataa kuachiwa mashimo na urithi kuchukuliwa na mataifa mengine.

“Hata Biblia inasema tutangulize yaliyo mema hata kama una hasira naye, hata Yesu Kristo alipokuwa anatoa ujumbe kwa makanisa saba alikuwa anaanza kupongeza mazuri hata kabla ya kuinua jambo lolote la kupinga, atakayekuwa anapinga atakuwa ni mkorofi na hata ukiwa na hoja itakuwa ngumu kusikilizwa,” amesema Askofu Kakobe.

Hata hivyo, Kakobe amemshauri Rais Magufuli kuwa anapoanza kupambana na suala hilo ni bora aanze kufanyiakazi kwanza fikra za watu kadri wanapozidi kutamka vitu vizuri.

 

Mnangagwa arejea nyumbani, adai hali ni shwari
DC Mjema apokea jengo la Ofisi ya Walimu kutoka Serikali ya Japan