Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa, idadi ya wagonjwa wa Covid -19 imepungua kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamebaki wagonjwa wanne pekee ambao wapo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Licha ya kutoa taarifa hiyo, Waziri Ummy ametoa wito kwa watanzania kuwa takwimu hizo zisiwasahaulishe kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugojwa huo.

Ameyabainisha hayo leo Juni 1, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ya uzinduzi wa jengo la Bodi ya Mkonge lililopewa jina la Mkonge House lililopo mkoani Tannga.

“Hapa Tanga hatuna mgonjwa wa Corona, DSM katika Hospitali ya Amana wamebaki 3, Mloganzila 1, Kibaha hatuna mgonjwa, Mwanza hatuna mgonjwa jambo la kusisitiza ni kuwa Corona bado ipo tuendelee kujikinga” Amesema Mwalimu.

Aidha amebainisha kuwa baada ya mlipuko wa virisi vya korona kufika nchini Tanzania, kwake ulikuwa ni wakati mgumu sana wa kufanya kazi.

“Nilisema pale Ikulu Dodoma katika Uwaziri wangu sikuwahi kupitia kipindi kigumu kama hiki cha Corona kwakweli nilihenya” amesema Waziri Ummy.

IGP Sirro: Hatutaki kutumia mabomu Uchaguzi Mkuu
Mkurugenzi GSM aahidi kuifanyia makubwa Young Africans