Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), limetoa orodha ya viwango vya soka duniani kwa mwezi Julai huku Tanzania ikipanda kwa nafasi 13  licha ya kutocheza mchezo wowote tangu ilipofungwa na Misri tarehe 4 Juni.

Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 136 mwezi uliopita hadi nafasi ya 123 dunani huku ikishika nafasi ya 33 barani Afrika.

Kwa nchi za Afrika Mashariki ambayo ni taifa pekee la ukanda wa CECAFA lililosalia katika mbio za kuwania kufuzu Kombe la Dunia imeendelea kwa kupanda nafasi 3 na sasa kushika nafasi ya 14 na 69 duniani.

Afrika nchi ya Algeria imeendelea kuongoza huku ikiahika nafasi ya 32 duniani,  Ivory Coast inashika nafasi  ya 35 na Ghana ikiwa nafasi ya tatu  na nafasi ya 36 duniani.

Kwa dunia, Argentina imeendelea kushika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Ubelgiji na Colombia katika nafasi ya pili na tatu.

Medeama SC Wabadili Mbinu Za Kuwasili
Waziri Mkuu Apokea Msaada wa Madawati 500 Kutoka China