Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji na ufanyaji wa biashara nchini, ambapo keasasa tayari muswada kuhusu mapendekezo ya Sheria mpya ya Uwekezaji umeshasomwa bungeni hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Jukwaa la Pili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililowashirikisha wadau mbalimbali wa biashara na uwekezaji kutoka Tanzania na Italia.

Makamba ashiriki warsha mradi uchakataji gesi asilia

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, akifungua Jukwaa la Pili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kijaji, ambaye alimwakilisha Rais Samia kwenye ufunguzi wa Jukwaa hilo amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira katika sekta ya biashara na uwekezaji ili kuwawezesha watanzania na wawekezaji kutoka nje kunufaika na fursa lukuki za biashara na uwekezaji zilizopo nchini.

Amesema, “Miongoni mwa maboresho hayo ni mapendekezo ya Sheria Mpya ya Uwekezaji ambayo tayari imesomwa Bungeni hivi karibuni, Sheria hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuwawezesha Watanzania wengi zaidikuwekeza kwenye miradi mikubwa ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.”

Baadhi ya wageni, wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Tanzania na Italia wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa a Jukwaa la Pili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania na wadau mbalimbali wa uwekezaji kutoa maoni yaokuhusu mapendekezo ya sheria hiyo ambayo tayari ipo wazi kwa umma wa watanzania kwa ajili ya kutoa maoni yao.

Maboresho mengine, yanayofanywa na Serikali kwenye Sekta ya Biashara na uwekezaji kuwa ni pamoja na kuanzishwa mifumo ya kiteknolojia inayomrahisishiamwekezaji namna ya kuanza biashara, kupata namba ya mlipa kodi, leseni, viza na vibali vya kazi na ukaazi. Kadhalika serikali inakamilisha kuandaa mfumo wa Kielektroniki kwa ajili ya kurahisisha utoaji mizigo bandarini.

Balozi Mulamula agusia utekelezaji Diplomasia ya uchumi
Makamba ashiriki warsha mradi uchakataji gesi asilia