Baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwa ni Pamoja na madini.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.

Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.

Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawaida na teknolojia.

Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa

 

 

 

Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.

”Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI” alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.

Video: Waziri Mkuu Majaliwa akizunguza baada ya kumaliza kikao cha SADC Botswana
Video: Airtel FURSA Yatoa Msaada Kwa Vituo Vya Yatima Dar