Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars kupoteza mchezo wake wa tatu mfululizo dhidi ya Algeria na kuondoa uwezekano wa kusonga mbele katika michuano ya AFCON lakini rekodi ya aina yake kwenye michuano hiyo.

Taifa Stars jana ilipoteza mchezo wake wa tatu mfululizo dhidi ya Algeria kwa kufungwa mabao 3-0 na kuingia kwenye orodha ya timu kutoka kwenye mataifa matatu ambayo yameshiriki michuano hiyo pasi na kuambulia alama hata moja.

Ukiachana na Tanzania ambayo haikuambulia hata alama moja katika AFCON mataifa mengine ni Namibia pamoja na Burundi ambazo nazo zimetoka kapa kunako michuano hiyo inayo fanyika nchini Misri.

Mbali na timu hizo kutopata alama zozote kwenye michuano hiyo lakini pia Taifa stars imekua timu ambayo imeongoza kwa kufungwa magoli mengi ambayo ni zaidi ya nane kati ya vikosi ambavyo vinawakilisha nchi zao kwenye michuano hiyo.

Julai 7 ya msanii Diamond Platnum ipo hivi
LIVE: Hafla ya Uwekaji Saini Miradi Mikubwa ya Maji jijini Dar es salaam