Denmark imesitisha krone milioni 65 ($9.8 milioni) ambazo zilikuwa ni msaada kwa Tanzania baada ya kutolewa kauli zisizokubaliana dhidi ya wapenzi wa jinsia moja (Ushoga) na mwanasiasa na kiongozi mwandamizi wa serikali.

Hatua hiyo ya Denmark imetangazwa na waziri wake wa Ushirikiano wa Maendeleo, Ulla Tornaes, ambapo hakumtaja kwa jina mwanasiasa mwandamizi wa Tanzania aliyetoa kauli hiyo ambayo wanasema haikubaliki na inashtusha.

“Nimeshtushwa na mambo hasi yanayoendelea Tanzania. hivi karibuni kuna kauli imetolewa isiyokubalika dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kiongozi mmoja wa kisiasa, kutokana na hilo nimezuia msaada wa DKK 65m kuelekea nchi hiyo. kuheshimu haki za binaadamu ni jambo kubwa na la muhimu kwa Denmark.”ameandika Tornaes katika ukurasa wake wa Twitter.

Aidha, Shirika la habari la nchi hiyo DR limeripoti kuwa, waziri huyo pia amesitisha ziara yake nchini Tanzania kutokana hatua zinazochukuliwa na viongozi kuhusu suala la ushoga.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitangaza operesheni dhidi ya wapenzi wa jinsia moja kwa kutaka watu wawaripoti polisi watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo,pia alitangaza kamati maalum ambayo pamoja na shughuli nyengine ingeliangazia suala hilo la wapenzi wa jinsia moja.

 

Hatua kali kuchukuliwa dhidi ya watakaoingiza bidhaa za magendo nchini
Spika Ndugai ampiga kijembe Msigwa 'Najua roho inamuuma sana'