Tanzania imeombwa kuisaidia Uturuki kiwango cha Tani 20 za Korosho kufuatia nchi hiyo kuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo yenye uhitaji zaidi nchini Uturuki, hivyo kupelekea kuomba msaada huo.

Ombi hilo limewasilishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara kutoka Uturuki ijulikanayo kama ‘Turkish Exportetrs Assembly’ (TIM), Kemal Batuhan Yazici ambapo amesema kuwa, kiwango cha korosho kilichopo nchini kimeshuka wakati mahitaji ya nchi ni Tani 20, hivyo wanaitegemea Tanzania kuondoa uhaba huo nchini mwao.

Amesema kuwa Korosho inayohitajika nchini Uturuki ni ile ambayo tayari imechakatwa na kufungashwa vyema kwa viwango vya kimataifa na sio malighafi hivyo ni vyema wafanyabiashara wakaandaa utaratibu wa haraka kuhakikisha Korosho zinasafirishwa kutoka Tanzania kwenda nchini Uturuki.

Aidha, Kemal amesema kuwa kwa muda wa miezi sita, kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Uturuki kimeongezeka kwa asilimia 9 kwa bidhaa za Tanzania zinazosafirishwa kutoka nchini Tanzania kwenda nchini Uturuki hivyo ongezeko hilo linaashiria Tanzania kupata soko lenye tija nchini Uturuki.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Katika siku za hivi karibuni nchi ya Uturuki imeongeza ushirikiano wake wa kibiashara na nchi ya Tanzania ambapo nchi hizo zimepata fursa mara kadhaa kuonesha maeneo yao ya uwekezaji baina yao ili kuongeza faida na kuleta maendeleo

Video: ADC walaani kufukuzwa waandishi wa TBC
Video: Majaliwa awaonya wapiga dili, asema cha moto watakiona