Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng.James Kilaba, alifanya mkutano wa kimataifa na wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na shirika la kimataifa la mawasiliano ITU kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa lengo la kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma.

Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.

“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” alisema.

Naye Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu alisema hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

“Hadi kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii inakua kwa kasi,” alisema.

“Malipo ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi hususani kwamba muda ndio muhimu,” yalisemwa na Profesa Ndulu.

Aliongeza kuwa “Mitandao ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account, mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo umepungua kwa sasa,”

 

Audio: Wema Sepetu - Sitaki kusikia 'team' Wema, Asema kama wanapenda wakamsapoti Idris
Mario Balotelli Apigiwa Chepuo La Kurudi England