Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) limeipatia serikali ya Tanzania mkopo wa Tsh. Bilioni 592.57 kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu ya kipaumbele ya umeme na maji.

Mikataba ya mkopo huo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, Balozi wa Ufaransa Tanzania, Frederic Clavier na Mkurugenzi Mkazi wa AFD, Stéphanie Mouen.

James amesema miradi hiyo inawiana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025, na inatekelezwa kupitia Awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II) 2016/17 – 2020/21.

Naye Mkurugenzi wa AFD, Mouen amesema Ufaransa imelenga kuisaidia Tanzania kufikia uchumi wa kati.

NEC yatangaza Asasi 272 zilizopita kushiriki uchaguzi Mkuu 2020
China yaibuka Mafua mapya ya Nguruwe, hatarini kuambukiza binadamu