Tanzania imepokea kwa heshima kubwa uenyekiti wa kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi ameishukuru Jamhuri ya Watu wa Namibia kwa kusimamia vyema nafasi hiyo kwa mwaka mzima uliopita.
 
Prof. Kabudi amepokea nafasi hiyo kutoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri linalojumuisha mawaziri wa nchi za Nje kutoka nchi wanachama wa SADC utakaodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uenyekiti wa Tanzania katika jumuiya hiyo.
 
Akizungumza wakati wa kupokea wadhifa huo, Prof. Kabudi amesema kuwa anaona fahari kwa kuwa nafasi ya Tanzania katika SADC ni ya kipekee kutokana na ushiriki wake katika kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
 
Aidha, Prof. Kabudi amesema kuwa nafasi hiyo ya uenyekiti wa mawaziri katika mkutano huo wa 39 wa SADC unakumbusha jukumu zito ambalo Tanzania ililibeba katika Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
 
Awali, mwenyekiti wa Baraza hilo alikuwa Naibu Waziri Mkuu wa Namibia anayeshughulikia Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa, Netumbo Ndaitwah, ambye nchi yake ndiyo iliyokuwa mwenyekiti wa mkutano wa 38 wa SADC, ambayo inamaliza muda wake rasmi wiki hii.
 
Amesema kuwa kumbukumbu hiyo inabebwa katika maeneo ya Kongwa, Nachingwea, Mgagao na Mazimbu ambayo yaliwahifadhi wapigania uhuru wa Msumbiji, Namibia, Botswana, Angola na Afrika Kusini ambao walipata hifadhi na mafunzo kwa ajili ya kwenda kuzikomboa nchi zao.
 
“Hakika, Umoja wetu katika SADC ndiyo nguvu yetu. Wakati huu tunapofanya mkutano huu wa 39 tunakumbuka pia miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere, ambaye alichangia kiasi kikubwa katika kuanzishwa kwa umoja huu,”amesema Prof. Kabudi.
 
Pia Prof. Kabudi amesema kuwa hakuna nchi inayoweza kujitegemea yenyewe katika kufikia adhma hiyo kwasasa, hivyo ushirikiano huo utasaidia katika kuweka na kusimamia sera wezeshi kwenye uwekezaji na ujenzi wa viwanda katika nchi za SADC kwani zinahitajika sera wezeshi na kuondoa vikwazo vya kibiashara katika maeneo yote ya nchi wanachama.
Awali, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, Ndaitwah ameeleza kusikitishwa kwao na ajali ya mlipuko wa Lori la mafuta mkoani Morogoro na kusababisha zaidi ya vifo vya watu 69, kisha kutoa pole kwa Serikali ya Tanzania.
 
“Tunashukuru pia kwamba nchi sita ambazo ni ESwatini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jamhuri ya Madagascar, Muungano wa Comoros, Jamhuri ya Malawi na Jamhuri ya Afrika Kusini kwakuwa zimefanya uchaguzi huru na wa haki wa kidemokrasia na kumaliza salama kwa amani
Dereva wa Lori lililopinduka apatikana
Serena Williams aubwaga ubigwa kwa chipukizi wa Canada