Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA),  limetangaza viwango vipya vya ubora wa soka duniani kwa mwezi Juni, 2016 huku Tanzania ikiporomoka.

Tanzania iliyotoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Kenya, imeporomoka kwa nafasi saba na kutua nafasi ya 136.

Katika orodha hiyo iliyotolewa leo, Argentina bado wapo kileleni wakifuatiwa na Ubelgiji, na Colombia, iliyopanda hadi nafasi ya tatu.

Uganda wanaendelea kuongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati wakisalia katika nafasi ya 72 duniani,  wakifuatwa na Rwanda (103), Ethiopia ( 125) Sudan ( 128), Kenya ( 129), Burundi ( 132) na Tanzania ( 136).

Katika 10 bora barani Afrika, Algeria inaoongoza ikifuatiwa na Ivory Coast na Ghana katika nafasi ya pili na ya tatu .

Wapinzani wa Tanzania katika pambano la Jumamosi la kuwania kufuzu kucheza AFCON, Misri wameporomoka kwa nafasi moja na kushika nafasi ya 5 barani Afrika.

Mabondia Wa Kulipwa Waruhusiwa Kushiriki Olympic
Ilkay Gundogan Ajiunga Rasmi Na Man City