Pembezoni mwa Mikutano ya Maji ya Umoja wa Mataifa inayoendelea New York Marekani Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameshiriki katika mjadala wa Uongozi na Usimamizi wa Masuala ya Maji.

Katika mchango wake, Aweso alisema Tanzania ipo katika agenda ya kuongeza msukomo na utashi wa kisiasa, bajeti ya maji na kuimarisha taasisi zinazohusiana na usimamizi wa huduma za maji na utekelezaji wa Miradi ya Maji.

Amesema, Tanzania inatekeleza Programme ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu yenye thamani ya Doal za Kimarekani Bilioni 6.47 na mwezi Mei 2023 itazindua Programu ya Uwekezaji katika Sekta ya Maji (Tanzania Water Investment Programme 2023-2030).

Mjadala huo, ulihudhuriwa na mgeni Rasmi Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa GWPSA na Mwenyekiti mwenza wa Jopo la Viongozi Maafuru kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Maji.

Meridianbet Yafika Fire-Kariakoo Kuzindua Duka Jipya
Wizara Madini, Maliasili kuandaa miongozo uchimbaji Hifadhini