Timu ya Wasichana ya Tanzania inayoshiriki fainali za Kombe la Dunia kwa watoto walio kwenye mazingira magumu imefanikiwa kuingia fainali baada ya kuifunga timu ya taifa ya wasichana ya England bao 2-1 magoli hayo yakiwa yamefungwa na Mastura Fadhili na Asha Omari katika mchezo wa nusu fainali uliomalizika asubuhi ya leo huko jijini Moscow Urusi.

Kikosi hicho kitapambana na Brazil katika fainali ya Kombe la Dunia la Watoto wanaoishi katika mazingira magumu itakayochezwa Jumatano, jijini Moscow nchini Urusi.

Watoto hao ni kutoka Kituo cha TSC Jijini Mwanza ambao watacheza fainali dhidi ya wasichana wa Brazil ambao nao wamefuzu fainali hiyo.

Tanzania ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo la dunia kwa mwaka 2014 nchini Brazil ambapo timu ya wavulana walio kwenye mazingira magumu ilichukua ubingwa kwa kuifunga Burundi.

Katika hatua za makundi, Tanzania ilicheza na timu za Urusi, Kazakhstan na Marekani katika hatua ya robo fainali na kisha leo kuitoa England kwenye nusu fainali.

Wilfried Zaha: Siendi popote
Keita kutua Anfield kwa dau hili