Tanzania imeporomoka kwa nafasi tano kwenye viwango vya shirikisho la soka duniani, FIFA kwa mwezi Novemba.

Taarifa iliyotolewa na FIFA leo inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka ya 142 mwezi Oktoba, wakati Uganda imeendelea kuongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani – na Senegal inaendelea kuongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 FIFA.

Katika 10 Bora mwezi huu Ujerumani bado inaongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.

Msando amshukuru JPM
Romario kuwania kiti cha urais wa soka Brazil