Mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) amepata pigo kwa kuondokewa na baba yake mzazi, Mzee Rashid Mkwachu leo Julai 19, 2018.

Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya familia, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa Mzee Rashid amefariki leo na shughuli za mazishi zitakuwa Msasani nyumbani kwa Dkt. Kikwete.

Ridhiwani pia ameeleza kuwa mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kisutu saa kumi jioni baada ya sala ya alasiri.

“Kwa niaba ya Familia ya Mama Salma Rashid-Kikwete na Dr. Jakaya Kikwete, naomba kutoa taarifa kuwa Mama Salma Rashid Kikwete amefiwa na Baba yake Mzazi Mzee Rashid Mkwachu.”

Dar24 Media tunatoa pole kwa wafiwa wote na Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali Pema Peponi, Amen.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Julai 20, 2018
Hamisa atii amri awapigia magoti watanzania

Comments

comments