Mzazi wa msanii nyota wa Bongo fleva, Belle 9, mzee Damian Nyamoga amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Meneja wa Belle 9, Jahz Zamba, zimeeleza kuwa Mzee Damian amefariki dunia baada ya kugongwa na boda boda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro alikokuwa anaishi.

Zamba amesema mzee Damian alivunjika mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa hospitali. Amesema baada ya Mzee Damian kupelekwa hospitali na kuwekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahtuti, kuna dawa zilikuwa zikihitajika lakini zilikosekana kwenye hospitali hiyo.

Naye rafiki wa karibu wa Belle 9, Lulu Diva amesema kuwa mzee Nyamoga amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa katika Hospitali baada ya kuwahishwa kwa ajili ya matibabu kufuatia ajali hiyo ya kugongwa na pikipiki wakati anavuka barabara.

Timu nzima ya Dar24 imepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa na inatoa pole kwa familia ya msanii huyo na Mungu awape moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mzee Nyamoga.

Video: Majaliwa atoa agizo NEEC, Ataka ripoti kabla mwezi Mei, 2018
Ben Pol kufanya kazi na 'Producer' mkubwa Marekani