Mbunge wa Mikumi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay amepata pigo kubwa ambapo amefiwa na baba yake mzazi leo akiwa katika Hospitali ya St. Kizito,  Mikumi, ambapo alikuwa asafirishwe kwenda kupata matibabu zaidi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Prof. Jay amethibitisha kifo hicho katika mawasiliano aliyoyafanya kwa njia ya simu akiwa Dodoma.

Aidha viongozi mbalimbali kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wametoa salamu zao za pole kwa Mbunge huyo na kumwombea kwa Mungu amtie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Timu nzima ya Dar 24 inatoa pole kwa familia ya Joseph Haule kwa kupotelewa na mpendwa wao.

Video: Tazama ulinzi wa Trump ulivyo mkali, Barack Obama haingii ndani
Kocha Tite amkabidhi kitambaa Neymar

Comments

comments