Diwani wa kata ya Kimwani iliyoko Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, Silvester Miga (CUF) amepoteza maisha baada ya kuvamiwa na kukatwa na mapanga nyumbani kwake, usiku wa kuamkia jana.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, , Augustine Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa marehemu alipoteza maisha majira ya saa saba usiku akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Kagondo.

Marehemu Augustino Sylvester Muliga

Marehemu Augustino Sylvester Muliga

Imeelezwa kuwa Miga alivamiwa nyumbani kwake akiwa anaangalia taarifa ya habari kwenye runinga ambapo watu hao walimvamia na kutekeleza tukio hilo la kikatili.

Kamanda Ollomi alisema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo limeendesha msako mkali na kuwakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo. Aliwataja watu hao kuwa ni Aderarid Antony mwenye umri wa miaka 42 na Shiranga Gonzari mwenye umri wa miaka 22.

Baadhi ya wakazi wa kata Kimwani waliwaambia waandishi wa habari kuwa mazingira ya kuuawa kwa diwani wao ni ya kisiasa zaidi.

WHO yatangaza hali ya hatari duniani kwa ugonjwa wa Zika sawa na Ebola
Mke wa Kafulila aibuka na ununuzi wa Mabehewa Mabovu Bungeni, Mwakyembe aweka rehani ubunge wake