Mtangazaji maarufu nchini, Isaac Gamba aliyekuwa akifanya kazi zake za utangazaji katika kituo cha DW cha nchini Ujerumani amefariki dunia akiwa nyumbani kwake.

Akizungumzia tukio hilo, mmoja ya watangazaji wa kituo hicho, Mohammed amesema kuwa Gamba hakuwasili kazini kwa siku mbili mara baada ya kumaliza likizo yake, ndipo wafanyakazi wenzake walipoamua kumtafuta katika sehemu anazopendelea kwenda, hatimaye kumkuta nyumbani kwake akiwa tayari amefariki dunia.

Amesema kuwa taratibu za msiba bado zinaendelea, aidha ndugu wa marehemu tayari wamepewa taarifa juu ya msiba huo.

“Gamba alikuwa ni mtu ambaye anapenda kazi yake Gamba alikuwa ni mtuwa  kuchanganyika, ni pigo kubwa kwa idhaa hii ya kiswahili” Amesema Mohammed

Aidha taratibu zote zitatolewa mapema kesho.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 19, 2018
Diddy, Cassie wapigana chini

Comments

comments