Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman amefariki ‪dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar‬ es Salaam.

Machi 16, 2019 Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alimtangaza Khalifa ambaye alikua mbunge wa zamani wa Jimbo la Gando, kuchukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad katika makao makuu ya CUF jijini Dar es Salaam.

Marehemu Kahalifa ‪aliwahi kuwa Mbunge wa Gando (1995-2015) na alizaliwa Agosti 9, 1956‬‬.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kupumzishwa leo katika makaburi ya kisutu wilayani Ilala jijini Dar es salaam.

Kifo cha kwanza mgonjwa wa Corona Tanzania
LIVE: Yanayojiri Bungeni leo

Comments

comments