Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Boutros Boutros Ghali amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 93.

Shirika la habari la Misri limeeleza kuwa Ghali alifariki akiwa katika hospitali ya Cairo alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kutokana na kuvunjika mfupa wa kiunoni.

Ghali alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kutoka Afrika alipoipata nafasi hiyo mwaka 1992 na kutumikia kipindi kimoja hadi Desemba 1996.

Mwanasiasa huyo raia wa Misri alipata umaarufu na heshima kubwa kufutia msimamo wake kuhusu vita ya Ghuba.

Kifo chake kilithibitishwa na Rafael Dario Ramirez Carreno ambaye ni Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Raia wa India anyooshwa baada ya kuwaita watanzania ‘Nyani’
Mwanamke Kusimamia Sheria 17 Za Soka Simba Vs Yanga