Mama mzazi wa msanii wa muziki wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, Bi. Martha Mbibo, amefariki dunia alfajiri ya leo.

Akithibitisha taarifa hizo kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, amesema kuwa mama yao amefariki akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Aidha, Dabo amesema kuwa msiba huo upo nyumbani kwa marehemu Jet rumo jijini Dar es salaam, na familia itatoa utaratibu wa mazishi mara baada ya utaratibu wa kuupeleka mwili hospitali kuhifadhiwa kukamilika.

JPM- Tutawashughulikia wote watakao uchezea Muungano awe Nje ya Nchi au Ndani ya Nchi
Mzee Majuto awatoa hofu mashabiki wake

Comments

comments