Mama mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini mkoani Tabora (CCM), Hussein Bashe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhumbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.

Kupitia akaunti yake ya Twitter Bashe ameandika hivi

”Ndugu zangu nimeondokewa na mama yangu mpendwa Inna Lillah wa inna ilayhi raji’un.

Naye Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe Ruyangwa ametumia kurasa wake wa Twitter kutoa salamu za pole kwa mbunge mwenza Bashe na kuandika hivi.

”Inna Lilah waina ilaiyhi raajiun. Mola akupe subra ndugu yangu Hussein Bashe katika mtihani huu mkubwa wa kufiwa na mama yako mzazi. Poleni sana Sheikh Mohammed, Ibrahim Mohamed Bashe, Abubakar, Kauthar na ndugu na jamaa huko Nzega. Tupo pamoja na nyinyi na Mola awape nguvu.

Aidha, Timu nzima na uongozi wa Dar 24 unatoa salamu za pole kwa Mbunge wa jimbo la Nzega Mhe. Bashe kwa kuondokewa na mama yake mzazi, Mungu aipumzishe roho ya marehemu kwa amani.

Endelea kufuatilia Dar24 tutaendelea kukujuza taarifa zaidi juu ya msiba huu.

Pusha T amvuruga Drake, alazimika kujieleza mtandaoni
Kujipima ukimwi nyumbani kwazua sura mpya