Mapacha wawili walioungana, Maria na Consolata wamefariki dunia usiku wa Juni 2, 2018 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa walikokuwa wakipatiwa matibabu.

Mapacha hao wamekuwa wakifanyiwa uchunguzi tangu mwishoni mwa mwaka jana, mara kadhaa baada ya kupata matatizo ya moyo.

Zikiwa ni juhudi za kutafuta suluhu ya ugonjwa wao, mapacha hao walifikishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam kupatiwa matibabu ya moyo ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ni miongoni mwa viongozi walioenda kuwajulia hali wakiwa hospitalini hapo.

Dar24 Media tunaungana na watanzania wote kuwaombea wapumzike kwa amani, Amen.

Video: Ofisa alipwa mshahara mara 10 zaidi ya JPM, Ngeleja, Kalamagi, Yona watajwa tena
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Juni 3, 2018