Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, na mbunge wa sasa wa jimbo la Muhambwe, Kigoma Atashasta Nditiye, amefariki dunia katika hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo chake imetolewa Bungeni leo Februari 12, 2021, na Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambapo ameeleza kuwa kifo hicho kimekuja baada ya kupata ajali siku ya Jumatano Februari 10 katika eneo la Nanenane Dodoma. 

Kufuatia kifo cha mbunge huyo, Spika Ndugai, ameahirisha shughuli za Bunge hadi kesho Jumamosi wakati itakapotolewa taarifa za taratibu za kuaga mwili na maziko.

Bwalya: Nitalipa kisasi
Gomes: Ninamfahamu vizuri Ibenge