Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Hafsa Mossi wa Burundi ameripotiwa kuuawa na watu wasiojulikana, mjini Bujumbura.

Kwa mujibu wa BBC, Mossi aliuawa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni mjini humo.

Msemaji wa Rais wa Burundi, Willy Nyamitwe ameeleza kusikitishwa na tukio la kuuawa kwa mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Burundi.

Viongozi wa ngazi za juu wa Burundi wamelaani kitendo hicho cha mauaji kupitia mtandao wa twitter. Naye Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo, Alain Aime Nyamitwe ametoa pole kwa familia, Serikali na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Billnass anahitaji Mwanamke Mwenye Hofu ya Mungu, Vipi kuhusu Linah!!
Naibu Waziri Mpina Akitoza Faini Ya millioni Kumi Kiwanda Cha MMI steel Kwa Uchafuzi Wa Mazingira