Aliyewahi kuwa waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Idd Mohamed Simba amefariki dunia katika hospitali ya JKCI Jijini Dar es salaam.

Licha ya kuwa Waziri chini ya uongozi wa Rais Benjamini Mkapa, Simba alikuwa Mbunge wa jimbo la Ilala kupitia tiketi ya CCM.

Akithibitisha kifo chake, Mtoto wake, Sauda Simba Kilumanga amesema kuwa Baba yake amefariki dunia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipatiwa matibabu.

kwa habari zaidi endelea kufuatilia Dar 24

Chelsea yajitosa jumla jumla kwa Hakim Ziyech
Muuguzi wa vyeti feki atuhumiwa kuua mwanafunzi

Comments

comments