Msanii wa bongo fleva Ilunga Khalifa, maarufu kama C Pwaa amefariki dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2021 akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Clouds fm, Ndugu wa karibu wa C Pwaa amethibitisha kuwa msanii huyo alikuwa anaugua Pneumonia na alifikishwa Hospitali kwa matibabu, ambapo hali yake haikuwa njema hadi hadi kufikwa na umauti.

Itakumbukwa enzi za uhai wake marehemu C Pwaa alifanya vizuri akiwa na kundi la Park Lane pamoja na Suma Lee walingara na wimbo kama Aisha, ambapo alifanikiwa kutoa nyimbo zake nje ya kundi ikiwemo Action, Problem, So Pwaa, Six in the Morning .nk.

Watanzania tuongeze juhudi katika hili
Waziri aagiza watumishi wa TBA kukamatwa