Beki wa mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara na nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub maarufu kama Cannavaro amepata pigo baada ya kufiwa na mwanae, Anuary Nadir ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Mwanaye ambaye alikuwa bado mchanga mwenye umri wa miezi miwili amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam

Msiba umetokea wakati beki huyo akipambana kuitumikia klabu yake iliyoko nchini Shelisheli kucheza mechi za kimataifa.

Cannavaro anatarajia kuwasili nchini leo akitokea Shelisheli ambako amekwenda kuitumikia Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya St Louis.

Salamu za pole ziwafikia wazazi wa mtoto huyo na ndugu wa karibu wa Annury Nadir, Mungu aipumzishe roho ya malaika huyo mahali pema peponi.

 

 

 

 

Polisi yakana kuhusika kukamatwa kwa mwandishi wa habari
Viongozi wa dini na siasa waomba kukutana na Rais