Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imepata msiba wa mtoto wao Rosemary Nyerere aliyefariki jana jioni jijini Dar es Salaam.

Kifo cha Rosemary kimethibitishwa na baadhi ya Wanafamilia akiwemo Sophia Nyerere na Manyerere Jacton.

Mmoja wa wanafamilia aliyejitambulisha kwa jina la Sophia Nyerere ameandika katika mtandao wa Instagram kuwa shangazi yake amefariki.

Taarifa zaidi kuhusu msiba zitatolewa hapo baadaye na Familia ya Marehemu. Rosemary ni miongoni mwa watoto saba wa Baba wa Taifa.

TRA yavunja rekodi ya makusanyo
Bernard Membe aihama ACT- Wazalendo