Mwanamuziki nguli wa Kenya, Achieng Abura alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta jijini Nairobi.

Abura alikuwa amelazwa kwa muda mrefu katika hospitali hiyo akitibiwa ugonjwa ambao haukuwekwa wazi.

Kwa mujibu wa The Standard, hali ya mwanamuziki huyo ilibadilika ghafla na akahamishiwa kwenye wodi maalum ya watu mahututi (ICU).

Kabla ya kulazwa hospitalini hapo, Abura ambaye aliwahi kuwa principal wa mashindano ya kuimba Afrika Mashariki ya Tusker Project Fame, aliwaaambia mashabiki wake kuwa alikuwa anaumwa na kwamba madaktari walimshauri kuongeza uzito na kasha kuupunguza tena.

Wasanii wa Afrika Mashariki wameonesha jinsi walivyoguswa na msiba huo, kwa kuandika jumbe mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii.


Dar24 inatoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na wadau wote wa muziki Afrika Mashariki . Apumzike kwa Amani. Amina!

Audio: Taarifa ya Polisi Tanga kuhusu kukamatwa majambazi waliovamia chuo kukuu.
TFF: Yanga Walikua Sahihi Kumtumia Hassan Kessy