Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Pancras Ndejembi amefariki dunia leo Jumamosi Desemba 29, 2018 majira ya saa 3:30 asubuhi.

Ndejembi amefariki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopelekwa kwaajili ya matibabu baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Aidha, mtoto wa Marehemu, Edna Ndejembi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema baba yake alikuwa anasumbuliwa na kifua kubana ambapo alilazwa katika Hospitali ya DCMC ya jijini Dodoma na kuruhusiwa juzi Alhamisi akiwa ameimarika kiafya.

“Lakini jana jioni hali yake ilibadilika ghafla ndipo tukamkimbiza hapo hospitali ya mkoa na leo saa tatu asubuhi mzee ametutoka,” amesema Edna.

Hata hivyo, Mzee Ndejembi aliwahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini na baadaye akawa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma na mwenyekiti wa wenyeviti wa mikoa kwa miaka 20.

Tanesco yatoa neno kuhusu kukatika kwa umeme
Shirika la Utangazaji la Taifa 'TBC' lapewa ushauri wa bure