Mwenyekiti wa NLD, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Dkt. Emmanuel Makaidi amefariki leo majira  mchana katika hospitali ya Nangao mkoani Lindi.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Dkt. Makaidi ambaye alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Masasi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Dkt. Makaidi ni mgombea ubunge wa tano kufariki katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

Dar24 inatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa Dkt. Emmanuel Makaidi na taifa kwa ujumla.

Apumzike kwa amani. Amina!

FC Barcelona Kusaka Haki Yao CAS
How To Write A Custom Essay Using Metaphor