Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia.

Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.

Aidha, mwanzoni mwa mwezi Januari, Mke wa mzee Kingunge, Peras Ngombalemwiru alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.

Hali ya baba mzee Kingunge awali ilikuwa ikiendelea kuimarika kasoro miguu ambayo bado ilikuwa ikisumbua.

Dar24 Media tunatoa pole kwa familia na watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza mzee wetu Kingunge.

Tunamtakia mapumziko mema.

Walimu 'vicheche' wakalia kuti kavu
Magazeti ya Tanzania leo Februari 2, 2018