Mchekeshaji mkongwe nchini mzee Majuto amefariki dunia leo Agosti 8  saa mbili usiku huu baada ya kulazwa siku chache zilizopita katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mtoto wake aitwaye Abuu amethibitisha habari hizi. Pia, mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram.

“R.I.P @Kingmajuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu,” aliandika Joti.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu King Majuto mahali pema peponi.

Aidha, Dar24 inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki na wasanii wote wa filamu nchini kwa kumpoteza kiungo katika tasnia hiyo.

Mzee Majuto alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume, uliofanywa asafirishwe mpaka nchini India mara baada ya kufanyiwa upasuaji hapa nchini.

 

Courtois ang'oka Stamford Bridge, Kovacic aondoka Real Madrid
Esther Matiko ashikiliwa na Jeshi la Polisi

Comments

comments