Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefariki dunia, leo Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo.  

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais Magufuli, akieleza kuwa Mheshimiwa Rais alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mzena alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na tatizo la moyo.

“Tarehe 14 Machi alijisikia vibaya na akakimbizwa katika Hospitali ya Mzena, ambapo alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mpaka umauti ulipomkuta,” amesema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais ametangaza maombolezo kwa siku 14, ambapo bendera zitakuwa nusu mlingoti.

Taarifa za kifo cha Mheshimiwa Rais Magufuli zimepokelewa kwa masikitiko makubwa na Watanzania, ambapo kupitia mitandao ya kijamii na makundi ya Whatsapp wameonesha kushtushwa na taarifa hiyo mbaya.

Makala: Maisha ya Dkt. Magufuli, mwanga ulioing’arisha Tanzania umezimika
Wanaohujumu miuondombinu watangaziwa kiama