Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa amefariki dunia leo, Julai 24, 2020 katika hospitali ya jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amelitangazia Taifa kifo cha Rais huyo mstaafu na kuwataka watanzania kupokea taarifa hiyo na kumuombea.

“Kwa masikitiko makubwa tumepata msiba mkubwa, Mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu amefariki dunia, amefariki dunia katika hospitali Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa, niwaombe Watanzania tulipokee hili, tumepata msiba mkubwa na tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele za haki, taarifa zingine zitaendelea kutolewa lakini Mzee Mkapa hatunaye tena,” amesema Rais Magufuli.

Mzee Mkapa ambaye alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kaunzia mwaka 1995 hadi 2005, amefariki akiwa na umri wa miaka 81.

Historia ya Mkapa, Nyerere alivyomuamini, kumuibua Magufuli, mateso na furaha
Vijana wamchukulia Prof. Lipumba fomu ya Urais CUF

Comments

comments