Rais wa zamani wa Burundi, Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki katika hospitali ya ‘Saint Elizabeth’ iliyoko Brussels nchini Ubelgiji.

Taarifa za kifo cha Kanali Bagaza zimethibitishwa na Mshauri wa Rais wa Burundi, Willy Nyamitwe kupitia mtandao wa Twtitter. Nyamitwe amemtaja rais huyo wa zamani kuwa ‘alikuwa Seneta wa Maisha’.

Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi na kutawala kwa takribani miaka 10. Hata hivyo, Meja Pierre Buyoya, aliyekuwa binamu yake aliongoza mapinduzi mengine ya kijeshi yaliyomuondoa Kanali huyo madarakani mwaka 1987.

Dar24 inatoa pole kwa ndugu jamaa na wana Burundi kwa ujumla.

Forbes wataja wana hip hop matajiri zaidi duniani, Drake achomoza
Mousa Dembele Huenda Akafungiwa Kama Luis Suarez