Ikiwa imepita takribani wiki moja na siku kadhaa tangu Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kumpoteza mtangazaji wake, Marin Hassan Marin, Wafanyakazi wengine wawili wamefariki dunia jana April 11, 2020.

Imeelezwa kuwa mwandishi wa habari mwandamizi wa TBC Lutengano Haonga amefariki dunia jioni ya jana, katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Huku meneja wa TEHAMA wa Shirika hilo, Joseph Kambanga akiwa amefariki dunia katika hospitali ya Amana jijini DSM.

Marehemu Joseph Kambanga amezaliwa Novemba 30 mwaka 1963 na ameanza kazi iliyokuwa Radio Tanzania –RTD, na sasa TBC Novemba MOSI 1990.

Tangu kuajiriwa, Kambanga ameshika nafasi mbalimbali ndani ya shirika na hadi anafariki alikuwa meneja wa TEHAMA. Kambanga ameacha mke na watoto watatu.

Imeelezwa kuwa dugu wachache tu wataruhusiwa kuhudhuria mazishi ikiwa ni pamoja na mke wake na watoto wake. Wizara ya Afya itaratibu mazishi yake.

watu 91 waliopona Corona Korea kusini wamepata tena
Billnass: Nampenda sana Nandy, nimechagua pande zote mbili