Mke wa zamani wa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Mama Winnie Madikizela Mandela amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Msemaji wa familia, Victor Dlamini, amesema Winnie amefariki kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua kwa muda mrefu, ambao ulimfanya atumie muda mwingi hospitalini tangu mwanzo wa mwaka huu.

Winnie anakumbukwa katika historia ya Afrika Kusini kuwa mpiganaji na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi sambamba na Nelson Mandela.

Picha yake akiwa na Mandela inayowaenesha wakiwa wameshikana mikono muda mfupi baada ya Mandela kuachiwa huru kutoka kwenye kifungo alichokitumikia kwa miaka 27 inatumika kama ishara ya ukomo wa ubaguzi wa rangi uliokuwa umekithiri.

Winnie Mandela akiwa nje ya mahakama, siku ambayo mumewe alihukumiwa kifungo cha maisha jela

Mama Winnie alizaliwa mwaka 1936 katika eneo linalojulikana sasa kama Transkei. Alikuwa mfanyakazi katika sekta ya kijamii ambapo alikutana na Mandela mwaka 1950. Wawili hao walifanikiwa kupata watoto wawili wa kike.

Walitengana baada ya Mandela kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

 

Israel kuwagawa wahamiaji kutoka Afrika
Miguna asafirishwa kwenda Canada