Mbunge wa Kinondoni (CCM) Abbas Tarimba ameishauri Serikali ya Tanzania kulisafisha Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ili kuleta matumaini yaliyotarajiwa na wapenzi wa mchezo huo.

Tarimba ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 31, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo kwa mwaka 2021/2021.

“Leo huyu akifanya makosa yale yale anapona mwingine leo akifanya makosa yale yale anaadhibiwa kesho yake na adhabu za kutisha zaidi,”amesema.

“Malalamiko yanapelekwa TFF leo kesho yapatiwa majibu, mengine yanakaa miezi sita hadi saba, standard (usawa) iko wapi Napata mashaka ndani ya TFF hakuna uadilifu,”amesema.

Ameitaka Serikali kusafisha mpira wa miguu ili kuleta matumaini yaliyotarajiwa na kwamba mambo hayo yameathiri hata Timu za Taifa ambazo hazina matumaini.

Papa Francis amteua Padre Msimbe kuwa Askofu mpya Jimbo Katoliki la Morogoro
Simba SC kwenda Mwanza