Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) umeitaka jamii kushirikiana na serikali katika kuwabaini na kwatambua wananchi wenye uhitaji ili kuondoa udanganyifu katika utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya maskini awamu ya pili unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Wito huo umetolewa na mtaalamu wa utafiti na maendeleo kutoka mfuko wa maendeleo (TASAF) Tumpe Lukongo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa mafunzo kwa wakuu wa Idara na wawezeshaji wa ngazi ya halmashauri wilaya ya Bahi.

Ikumbukwe Uendeshaji wa wa zoezi hilo la uhakiki ni utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Rais Dkt. John Magufuli wakati akizundua TASAF III awamu ya pili Februari 17, 2020 ambapo alielekeza kufanyika uhakiki na kusafisha daftari la kaya maskini kabla ya kuanza utekelezaji.

”Tofauti na hali iyokuwa mwanzo sasa wananchi wamewezeshwa kwa kupewa mitaji ambayo imewasaidia katika kipato na kurahisisha maisha ya kila siku,” alisema Rais Magufuli

Pamoja na hayo Lukongo amesema uhakiki huo utafanyika kwa lengo la kupata orodha halisi kwenye masijala ya kaya za walengwa.

Ruksa wafungwa kutembelewa
Wanafunzi wanusurika kifo Bweni likiteketea kwa moto