Diamond Platinumz amewapa heshima ya aina yake wasanii wenzake wa Bongo Flava wanaofanya vizuri na waliosaidia katika kuung’arisha muziki huo hadi kufikia hapo, kwa kuwaweka ndani ya studio yake mpya ya kisasa ya WCB.

Msanii huyo ambaye mashabiki wengi wanaamini ana uhasama (beef) na Ali Kiba ambaye ni kaka yake katika muziki, ameonesha kuwa huenda kinachoonekana kwenye mitandao ya kijamii kwa mashabiki hao waliojenga timu kubwa mbili za majeshi yanayoshambuliana zikawa na muelekeo tofauti na uhalisia.

Katika kipande cha video alichopost meneja wa Diamond, Babu Tale kinaonesha ndani ya studio hizo kuna picha zinazoonesha wasanii kadhaa akiwemo ‘Ali Kiba’.

WCB Headquarter

A video posted by Hamisi Taletale (@babutale) on


Hii ni ishara nyingine ya kuyeyuka taratibu kwa uhasama unaotajwa kwani wiki kadhaa zilizopita, Ali Kiba aliwataka mashabiki kuhakikisha wanampigia kura Diamond Platinumz aweze kushinda tuzo za BET, tuzo ambayo bahati mbaya hakufanikiwa kuipata.

Kadhalika, katika kipindi cha hivi karibuni, Ali Kiba ameonekana katika picha kadhaa za pamoja na mameneja wa Diamond.

Kwa muelekeo huu, huenda tukaja kupata ‘collabo’ iliyo kwenye ndoto za mashabiki wengi kati ya wasanii hao ambao majeshi yao ya mashabiki (Team Diamond Vs Team Kiba) yamejihami na kushambuliana kwa nguvu mara kadhaa mitandaoni.

Video: Taarifa kutoka TRA kuhusu 18% VAT kwenye huduma za fedha
Hemed asimulia Maisha ya ‘uteja’ ya baba yake yalivyomfunza kuwa tofauti