1. Radamel Falcao.

Kutoka AS Monaco kwenda Chelsea.

Alikuwa na msimu mbovu alipokuwa Manchester United msimu uliopita licha ya kupewa nafasi kubwa ya kucheza. Aliishia kufunga mabao manne tu. Lakini Mourinho ameamua kumleta vivyo hivyo akiamini ataisaidia timu yake.

 

  1. Papy Djilobodji.

Pauni milioni 2.2- Kutoka Nantes kwenda Chelsea.

Ripoti mbalimbali kutoka nchini Ufaransa zinaeleza kuwa hakuna chochote ambacho beki huyo anaweza kuwapa Chelsea. Iliripotiwa kuwa alitaka kupelekwa katika vilabu mbalimbali vya Uingereza lakini alikataliwa licha ya bei yake kuwa ndogo. Kwa uwezo uwanjani wataalamu wanasema hana kiwango cha kuwashinda Zouma, Cahill au mlinzi mwingine yeyote wa Chelsea.

 

  1. Fabian Delph.

Kutoka Aston Villa kwenda Manchester City.

Mwanandinga huyu hana uwezo wa kuwashinda Yaya Toure, Silva, Fernadihno, Navas, Fernando, Sterling, Debruyne na hata Nasri, ndio maana mpaka sasa tunaweza kusema kuwa hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kwa City.

 

  1. Younes Kaboul.

Kutoka Tottenham Hotspur kwenda Sunderland.

Sunderland walikuwa na tatizo kubwa katika safu ya ulinzi msimu uliopita.

Waliruhusu magoli mengi sana ambayo yangeweza kuwasababisha kushuka daraja. John Oshea na Wes Brown kwa sasa wakati umeshaanza kuwatupa mkono, Sasa usajili wa Kaboul mwenye miaka 29, ambaye pia ni ni mwepesi wa kuapata majeraha ya mara kwa mara ni tatizo jingine.

 

  1. Bastian Schweinsteiger

Euro milioni 14. Kutoka Bayern Munich kwenda Manchester United

Bastian Schweinsteiger anaweza kuwa moja ya wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika klabu ya Manchester United kwa msimu huu, lakini sio wa kucheza katika kikosi cha kwanza kwa dakika zote .

Kwa sasa Bastian ana umri wa miaka 30. Mechi dhidi ya Swansea na Newcastle zilithibitisha hilo. Badala yake Bayern Munich waliamua kumsajili Arturo Vidal kuziba pengo lake, Vidal ni mchezaji ambaye United walikuwa wakihusishwa naye wakatika wa dirisha la usajili la mwezi January.

John Bocco Anamini Ushindi Ni Mapambano
Profesa Lipumba: Mimi, Dk Slaa Ndio Wapinzani